POWA255

POWA255's avatar
POWA255
npub1zkkl...6uwq
POWA 255 ni mpango wa elimu ya Bitcoin kwa njia ya mtu kwa mtu (peer-to-peer) unaolenga kusambaza maarifa ya Bitcoin kwa kutumia lugha ya Kiswahili.
Tarehe 23/01/2026, POWA 255 na @Bitcoin Arusha kwa kushirikiana na @Hedhi Huru | Reusable Pads and Bitcoin Education walifanikisha mpango wa Reusable Menstrual Pads. Katika mpango huu, pedi zinazoweza kutumika tena zilitengenezwa na kugawiwa kwa wanafunzi takribani 42 wa Shule ya Sekondari Manushi, iliyopo Moshi, mkoa wa Kilimanjaro. ♻️📦 Pedi hizi zitawasaidia wanafunzi kuendelea kukaa shuleni kipindi chote cha hedhi kwa hadi miaka mitatu, bila vikwazo wala kukosa masomo. 🤝 Wewe pia unaweza kuwa sehemu ya mabadiliko haya Support kwa kumnunulia mwanafunzi mfuko mmoja wa pedi kupitia @Geyser